Chama cha upinzani CUF visiwani Zanzibar, kimewasilisha hoja binafsi kwa baraza la wawakilishi kikipendekeza kuundwe serikali ya umoja wa kitaifa.
Hoja hiyo imewasilishwa BUNGENI na Abubakar Khamis wa chama cha CUF.
Miongoni mwa mambo mengine yaliyopendekezwa ni pamoja na kufanyika kwa kura ya maoni mwezi Mei mwaka huu.
Vilevile kimependekeza baraza litoe agizo kwa serikali kukabidhi rasimu ya mabadiliko ya katiba ndani ya wiki moja.
Bw Khamis pia amependekeza marekebisho katika maeneo manne, mkiwemo nafasi ya waziri kiongozi kuchukuliwa na mshindi wa pili wa uchaguzi.
Kwetu news bulletin is there to update you on national and international news. This is there also to make your business well advertised inside and outside the country. The blogger is living Dar es salaam, Tanzania, Africa. Join us in order to be updated.
Friday, January 29, 2010
MASHAMBULIZI YA IRAQ YAMEELEZEWA NA BLAIR
Aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair anatarajiwa kutoa ushahidi mbele ya kamati inayochunguza kuhusika kwa Uingereza kwenye vita vya Iraq vya 2003.
Bwana Blair atahojiwa kwa muda wa saa 6 kuelezea sababu zake za kuunga mkono uvamizi wa Marekani nchini Iraq mwaka wa 2003.
Uingereza iliunga mkono vita hivyo kwa misingi kuwa Iraq ilikuwa na silaha za maangamizi makubwa. Blair anatarakiwa kueteta uamuzi wake kuwa rais Saddam Hussein alikuwa na uwezo na nia ya kuunda silaha za maangamizi ya halaiki.

Subscribe to:
Comments (Atom)