Wednesday, January 13, 2010

BBC BEST AFRICAN FOOTBALLER

Didier Drogba wa Chelsea na Ivory Coast ametangazwa mshindi wa tuzo ya mwanasoka bora wa BBC Afrika 2010.

Mshambuliaji huyo amepata kura zaidi kuliko Samuel Eto'o, Michael Essien, Yaya Toure, na Tresor Mputu Mabi kushinda taji hilo.

Matokeo ya kura - zilizopigwa na mashabiki kote Afrika yalitangazwa moja kwa moja kutoka Angola kupitia kipindi cha Fast Track katika Idhaa ya Kiingereza ya BBC.
Drogba yupo Angola akiiongoza nchi yake kujiandaa kwa michuano ya kombe la mataifa ya Afrika, ambako The Elephants wanapewa nafasi kubwa ya kushindwa.
Baada ya kuanza mwaka vibaya, Drogba aliimarisha kiwango chake cha soka na kuwa mmoja wa washambuliaji tishio duniani.
Baada ya kuwekwa kando kucheza kikosi cha kwanza na kocha Luis Felipe Scolari kutoka Brazil, mshambuliaji huyo alifunga goli moja tu katika mechi 10 ilipofika Februari

Waliowahi kushinda tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika

2008 - Mohamed Aboutrika
2007 - Emmanuel Adebayor
2006 - Michael Essien
2005 - Mohamed Barakat
2004 - Jay-Jay Okocha
2003 - Jay-Jay Okocha
2002 - El Hadji Diouf
2001 - Sammy Kuffour
2000 - Patrick Mboma




Tetemeko lasababisha maafa nchini Haiti

Maelfu wanahofiwa kufa kufuatia tetemeko hilo lililotokea nchini Haiti ambalo lilikuwa la kipimo cha 7.3 katika vipimo vya Ritcher.

Ripoti zinasema uharibifu mkubwa umetokea katikati mwa mji mkuu wa Port-au-Prince. Baadhi ya majengo yaliyoharibiwa vibaya ni ikulu ya rais na hospitali moja mjini humo.

Msemaji wa umoja wa mataifa mjini New York Martin Nesirkyo amethibitisha kuwa ofisi za umoja wa mataifa mjini Port-au-Prince zimeharibiwa. Amesema pia kuwa idadi kubwa ya watu wamezikwa chini ya vifusi na wengine kufa au kujeruhiwa.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hilary Clinton amesema Marekani tayari imeanza kutuma misaada ya dharura.
Wanajiolojia nchini Marekani wanasema tetemeko hilo la ardhi ndilo mbaya zaidi kwahi kuikumba Haiti kwa miaka mia mbili. Wataalamu hao pia wametoa tahadhari ya Tsunami.