The hugging day has nothing to do with human being but something about the feeling of human on a certain thing.
and this is not only for human but also for animals
Kwetu news bulletin is there to update you on national and international news. This is there also to make your business well advertised inside and outside the country. The blogger is living Dar es salaam, Tanzania, Africa. Join us in order to be updated.
Thursday, January 21, 2010
Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda Awaka Bagamoyo
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, ambaye kwa kawaida ni mpole na asiye na haraka, jana aligeuka mbogo wakati alipowavua madaraka viongozi wanne wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kutokana na kuhusishwa na tuhuma za ubadhirifu wa mamilioni ya fedha za maendeleo.
Katika kuonyesha kuwa hakukurupuka kufikia uamuzi huo mzito, Waziri Pinda alitangaza hapo hapo majina ya maofisa wengine waandamizi kutoka sehemu tofauti nchini ambao wameteuliwa kuja mjini hapa kuziba nafasi za waliosimamishwa.
Habari za kuwepo kwa ubadhirifu huo ziliripotiwa na Mwananchi wiki iliyopita wakati mpashaji habari mmoja alipodokeza kuwa Sh950 milioni zilizotengwa kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo, zilitafunwa na kwamba sakata hilo lilikuwa likimsubiri Waziri Pinda.
"Ndugu zangu suala la kukwamisha maendeleo ya wananchi ni kosa kubwa sana," alisema Pinda katika mkutano uliohusisha wadau mbalimbali wa maendeleo wilayani Bagamoyo.
"Sijui watu wanapata wapi jeuri ya kuyumbisha maendeleo... wanachota fedha huku, wanapeleka kule na kuchukua kule kuleta huku ili mradi vurugu tu."
Pinda alimvua madaraka mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Rhoda Nsemwa, ofisa kilimo, mifugo na ushirika, Naftari Mtula, ofisa mipango, Aloyce Gabriel, mkaguzi wa ndani, Abdul Mwinyi pamoja na mweka hazina wa wilaya Kalo, Wage.
Tuhuma nyingine zilizosababisha kuvuliwa madaraka kwa waandamizi hao ni kuwepo uzembe katika kusimamia na kufuatilia utekelezaji miradi, kutozingatia kanuni na sheria, kuwepo taarifa tofauti za utekelezaji miradi ya maendeleo pamoja na kutokuwepo kwa nyaraka sahihi za matumizi ya fedha za mwaka wa fedha wa 2008/2009.
Baadhi ya miradi ambayo imetajwa kukwama kutekelezwa katika kipindi hicho licha ya fedha kutolewa na serikali ni pamoja na mradi wa josho la Vigwaza, soko la matunda na nafaka la Kiwangwa, lambo la maji la Matuli, mradi wa umwagiliaji maji Bwilingu, kilimo cha pilipili na mradi wa vituo vya wanyama kazi.
Waziri Pinda, ambaye huonekana kuwa ni mpole na asiye na haraka, alisema viongozi hao wanne wamevuliwa madaraka yao hadi hapo uchunguzi utakapokamilika.
Alisema hatua zaidi zitachukuliwa baada ya taarifa ya uchunguzi kuonyesha kiwango ambacho watumishi hao wamehusika katika ubadhilifu, hatua ambazo ni pamoja na kufukuzwa kazi, kupunguziwa mshahara au kushushwa madaraka au kufikishwa mahakamani.
Waziri mkuu pia amemvua wadhifa mhandisi wa maji wa wilaya hiyo, Felis Ngomai ambaye atakuwa mtumishi wa kawaida kutokana na kubainika kuwa hana sifa ya taaluma hiyo, wakati ofisa elimu wa wilaya hiyo, Cheka Omari yupo chini ya uangalizi wa utendaji wake wa kazi kutokana na kuelezwa kuwa hakuwa msimamizi mzuri katika utekelezaji wa miradi ya elimu.
Pinda aliwaeleza wajumbe wa kikao hicho, ambacho kilihusisha madiwani, sekretarieti ya mkoa, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), pamoja na wabunge wote wa Bagamoyo, kuwa viongozi hao hawakuwa makini kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Waziri Pinda alitumia fursa hiyo kuwateua na kuwatangaza watendaji wapya watakaoziba nafasi hizo kuwa ni Samuel Salianga kutoka Kigoma Vijijini ambaye anakuja kuwa mkurugenzi mtendaji, Fidelis Nemetwa kutoka Shinyanga (mweka hazina) wakati ofisa mipango anakuwa Lucas Mweli kutoka Manispaa ya Moshi.
Wengine walioteuliwa jana ni Fidelis Nyevela kutoka Iringa ambaye anakuwa ofisa kilimo, Prudence Mtiganzi kutoka Kilombero (mhandisi wa maji), wakati mkaguzi wa ndani anakuwa Felista Masamba kutoka mkoani Lindi.
Uteuzi wao unaanza mara moja, kwa mujibu wa Pinda.
Wilaya ya Bagamoyo imekuwa ikikumbwa na malumbano baina ya watendaji wake kwa kile kinachodaiwa ni kutokuwepo kwa maelewano mazuri kati ya mkuu wa wilaya hiyo, Magesa Mulongo na mkurugenzi.
Habari zinadai kuwa mkuu huyo wa wilaya amekuwa akichunguza matumizi ya fedha za halmashauri, jambo ambalo limeelezwa kuwa linaudhi watendaji ambao wanadai kuwa madiwani ndio wenye wajibu wa kuhoji kila kitu.
Tuhuma hizo ziliilazimu serikali kumtuma mkaguzi mkuu kufanya uchunguzi wa uliobaini kuwepo mapungufu makubwa ya kiutendaji na upotevu wa mamilioni ya fedha.

JAMANI JAMANI
HATA WANYAMA WANAPENDA KUBUSU WATU ILA WANAPENDA PUA ZAID MAANA WANAONA KAMA NI PANYA FULANI HIVI.
See yourself this funny picture aven animals like to kiss human being.

Subscribe to:
Posts (Atom)