Monday, January 25, 2010

NDEGE YA ETHIOPIA YAANGUKA HUKO MEDITERRANEAN


Ndege ya abiria iliyokuwa imebeba watu 85 imeanguka katika bahari ya Mediterranean.

Ndege hio ilianguka muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Beirut nchini Lebanon.
Ripoti zinasema ndege hiyo aina ya Boeing 737 inamilikiwa na shirika la ndege la Ethiopia.
Maafisa mjini Beirut wanasema ndege hiyo ilipoteza mwelekeo takriban dakika 30 baada ya kupaa angani.
Watu wanaoishi karibu na bahari ya Mediterranean wameripotiwa kushuhudia ndege hiyo ikianguka baharini huku ikiwaka moto.
Inaaminika kuwa abiria 50 ni raia wa Lebanon huku wengine wakiwa raia wa Ethiopia.