Rais Obama ametangaza matokeo ya uchunguzi ulioendeshwa na ikulu ya Marekani kuhusu dosari za usalama kutokana na jaribio la raia wa Nigeria Umaru Farouk Abdul Mutallab la kuilipua ndege ya Marekani eneo la Detroit siku ya krisimasi.
Obama amesema serikali yake ilikuwa na taarifa muhimu za kuzuia shambulio hilo. Hata hivyo maafisa wa ujasusi walipuuza taarifa hizo na kuhatarisha nchi hiyo.
Rais huyo sasa ametangaza masharti mapya ambapo ameagiza taarifa zote za kiusalama zitolewe kwa vyombo vyote vya serikali.
Obama pia amesema yupo tayari kubeba lawama kosa linapotokea na kuongeza Marekani itaendelea kukabiliana na kundi la Al-Qaeda.
No comments:
Post a Comment