Katibu mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa Ban ki-Moon amesema kuwa anataka kupeleka wanajeshi na polisi 3500 zaidi kuimarishi utoaji wa misaada nchini Haiti, kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea wiki iliyopita.
Tayari shirika hilo liko na wanajeshi 9000 wa kulinda usalama waliopelekwa nchini humo miaka sita iliyopita, kuimarishi usalama wakati wa kipindi cha machafuko ya kisiasa.
Kwa sasa ujumbe huo unajiandaa kusaidia katika operesheni kubwa ya kibinadamu.
Maafisa wa kulinda amani wamesema kuwa uchunguzi wao umeonyesha kuwa hali ya usalama kwa ujumla imedhibitiwa. Lakini, wanajeshi zaidi wanahitajika kulinda misafara ya magari inayobeba misaada katika maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi.
Aidha, polisi wa ziada watasaidia kulinda vituo vya kusambaza misaada, lakini la muhimu zaidi ni kusaidia kuimarisha idara ya polisi nchini humo.

No comments:
Post a Comment